Michezo
Mwina Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ apata shavu nono Msimbazi, majukumu yake yaanza rasmi jana
Aliyekuwa kiongozi wa soka Tanzania na Katibu Mkuu wazamani wa Simba, Mwina Mohamed Kaduguda ameteuliwa na klabu hiyo kuwa Kaimu Mwenyekiti wa timu hiyo kuanzia hapo jana tarehe 19 Novemba 2019.
Kaduguda anachukua nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Swedy Mkwabi kufuatia kujiuzulu kwake, mbali na huyo Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya Simba Sports Club Limited imemteua Salum Abdallah Muhene kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Mwina Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ ambaye ni msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa sasa ni mwalimu katika shule ya Sekondari, Jitegemee jijini Dar es Salaam.