Michezo

Mashabiki wa Chelsea waliofanya vitendo vya kibaguzi wafungiwa maisha

Ghasia zilizotokea wakati mashabiki wa Chelsea walipokuwa nchini Ufaransa ili kushabikia mechi ya vilabu bingwa Ulaya kati ya Chelsea na Pasris Saint Germain tarehe 17 Februari, zimesababisha baadhi ya mashabiki kufungiwa kujihusisha na soka.

che1
Mashabiki hao wamefungiwa maisha na klabu ya Chelsea

Mkanda ya video ikimuonyesha raia mmoja wa Ufaransa, Souleymane Sylla ambaye ni mweusi, akisukumwa nje ya treni, kitendo ambacho hakikubaliki hasa katika michezo.

Mashabiki hao wanne wamefungiwa kuhudhuria mechi za soka kwa miaka mitano.

Richard Barklie, kutoka Carrickfergus, Northern Ireland, na Joshua Parsons na William Simpson, wote kutoka Surrey, walifungiwa kwa miaka mitano kwenye mahakama ya Hakimu ya Stratford.

Jordan Munday wa Sidcup huko Kusini Mashariki mwa London, alifungiwa kwa miaka mitatu. Waliambiwa hawatoweza kuhudhuria mechi kubwa za nyumbani na nje ya nchi. Chelsea pia imewafungia mashabiki hao kuhudhuria mechi zao maishani mwao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents