Tupo Nawe

Mastaboda ya NMB imekurahisishia malipo yako ya usafiri wa bodaboda

Mastaboda ya NMB imekurahisishia malipo yako ya usafiri wa bodaboda

Sasa Mastaboda imekurahisishia malipo yako ya usafiri wa bodaboda. Kwa kufuata hizi hatua chache, utakuwa umefanya malipo yako kimasta zaidi. Washtue na washkaji mtaani. #NMBMkononi #mastaboda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu nchini Tanzania, Jenista MhagamaWaziri Jenista anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,  alizindua kampuni hiyo, mapema mwaka huu ambapo alisema mfumo huo unaowawezesha abiria na wateja wake kulipa nauli kwa kutumia simu za mkononi na fedha hizo kwenda moja kwa moja kwenye akaunti ya NMB ya dereva husika.

Amesema Serikali inatambua uwapo wa kundi kubwa la vijana linalojishughulisha na shughuli hiyo halali akieleza kuwa ni wakati sasa kwao kujiunganisha na taasisi nyingine rasmi kama benki.

Amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa benki na taasisi za kifedha pamoja na kuchukua hatua pale zitakapoonekana changamoto zinazokabili teknolojia mpya zinazowawezesha vijana kujiajiri.

“Kuwa na fedha ni jambo moja ila namna ya kuzitumia ni jambo lingine, kuna haja ya mafunzo kutolewa kwenu yatakayowaongoza katika matumizi mazuri ya fedha kwa ajili ya maendeleo ya sasa na baadae.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW