Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Matic aeleza walichoambiwa na Mourinho wakati wa mapumziko baada ya kufungwa 2-0

Kiungo wa klabu ya Manchester United, Namanja Matic, ameweka wazi kile walichoambiwa na kocha wao Jose Mourinho wakati wa mapumziko baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Crystal Palace.

Matic akiongea baada ya mchezo huo amesema, kocha huyo aliwaamuru waongeze nguvu ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.

“Baada ya kufungwa goli la pili ilikuwa ngumu sana kwetu kurudi. Tulionyesha na tufanya kile meneja alitaka tufanye. Yeye [Mourinho] atuambia wakati wa mapumziko kuwa tunahitajika kuongeza nguvu zaidi,” amesema Matic.

“Ninafurahi nimefunga goli langu la kwanza Manchester United, najua si kazi yangu lakini ninafurahi kutupatia pointi tatu,” ameongeza.

Katika mchezo huo Man United waliibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW