Michezo

Mayanja aikacha Simba SC

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba, Jackson Mayanja ameamua kutangaza rasmi kuachana na timu hiyo hii leo kufuatia kukabiliwa na matatizo ya kifamilia.

Mayanja ambaye ni raia wa Uganda amesema tayari ameshafikia makubaliano na uongozi wa klabu ya Simba na muda wowote atarudi nchini kwao kuungana na familia yake.

“Nashukuru uongozi wa Simba SC, mashabiki na wachezaji wote ambao ninafanya nao kazi baada ya kufikia makubaliano wakiniruhusu niondoke nitaondoka nikamalizane na matatizo yangu ya kifamili,”amesema kocha Mayanga ambaye alishatabiriwa kuondoka katika timu hiyo toka mwanzo mwa msimu.

Uongozi wa klabu ya soka ya Simba SC kupitia kwa Afisa habari wake, Haji Manara amesema wamemalizana na kocha Mayanja kiungwana.

“Ametuahidi siku atakapo amua kurudi kufanya kazi nchini Tanzania kipaumbele chake cha kwanza itakuwa klabu ya Simba tunamtakia kila lakheri kwanza katika kutatua matatizo yake lakini pili katika taaluma yake ya ukocha popote pale atakapo jaaliwa kufanya kazi katika siku chache zijazo tutaangaza mbadala wake.” Amesema Sande Manara

Kocha huyo aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda chini ya kocha Bobby Wiliamson, amedumu Simba kwa misimu miwili akitokea Coastal Union, ambapo hakufanya vizuri sana lakini wakati anatua Simba kuchukua nafasi ya Dylin Kerr, Simba ilikuwa haifanyi vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents