Michezo

Mayweather ampa kiburi cha fedha McGregor

Maisha ya bondia Conor McGregor yamebadilika kabisa kwa sasa toka alivyopigana na Mmarekani Floyd Mayweather katika pambano la kihistoria na lililoingiza fedha nyingi.

Gregor amekuwa akiishi maisha ya kifahari na yagharama tangu alipotengeneza mkwanja mnene wa paundi milioni 100 kutoka katika pambano lake, ambapo hapo jana siku ya Jumatatu amekodisha ukumbi wa starehe wa Funderland amusement park kwaajili ya kufurahi yeye, familia yake na marafiki zake huku akionekana kuvalia vazi lenyethamani ya paundi 1,785.

Eneo hilo ambalo ni maarufu na linalovutia watu wengi kwa matembezi hasa nyakati za kipindi cha baridi bingwa huyo wa UFC na anayetambulika kama mwanamichezo anayependwa na mfano wa kuigwa nchini kwao Ireland alilikodisha kwaajili ya matanuzi.

“Nimeufungua usiku huu wa Funderland kwaajili ya familia na marafiki zangu kusherehekea kwa pamoja ‘fresh January Monday’,” amesema mwanamasumbwi huyo mwenye umri wa miaka 29.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents