Soka saa 24!

Mayweather ‘Money’ akana kutaka kuzipiga na dogo wa miaka 20 raia wa Japan ‘Sikuwa na makubaliano rasmi’

Bondia wa Marekani, Floyd Mayweather amekanusha taarifa za kukubali kupigana na mwana ‘kickboxer’ wa Japan, Tenshin Nasukawa.

Image result for mayweather vs Japan

Bingwa huyo wa Dunia, Mayweather ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Mayweather mwenye umri wa miaka 41, ambaye inasemekana alikuwa akitarajiwa kupigana na Tenshin mwenye umri wa miaka 20 Desemba 31 mwaka huu jijini Tokyo amekanusha habari hizo hapo jana siku ya Jumatano.

Image result for mayweather vs Japan

Sasa nipo narejea Marekani baada ya safari yangu ndefu na yenye kukatisha tamaa ya Tokyo, nafahamu nina muda wa kukufahamisha wewe shabiki yangu na vyombo vya habari kuhusiana na pambano langu lijalo Desemba 31 ambalo lilitangazwa.

”Sasa narejea Marekani baada ya safari ndefu ya kukata tamaa ya Tokyo, sasa nina wakati wa kukufahamisha wewe, mashabiki wangu na vyombo vya habari kuhusiana na tukio lijao tarehe 31 Desemba ambayo ilitangazwa hivi karibuni. Kwanza kabisa, nataka iwe wazi kwamba mimi, Floyd Mayweather, sikukubaliana rasmi,” amesema Mayweather.

Floyd Mayweather ameongeza “Kwanza kabla ya yote ningependa kuweka wazi kwamba mimi Floyd Mayweather, sikuwa na makubaliano rasmi ya kupambana na Tenshin Nasukawa. Kwa kweli kwaheshimazote niseme kuwa sijawahi kusikia habari zake hadi niliposafiri Japan,  niliombwa kushiriki maonyesho kwa dakika tisa tu ya ufunguzi wa Rizen Fighting Federation. Hicho ndicho nilichofahamishwa hapo hawali na Brent Johnson wa”One Entertainment”.

Hata hivyo katika maelezo yake bondia huyo aliyepambana mapambano 50 pasipo kupoteza hata moja amewaomba radhi mashabiki wake waliyokuwa wamejiandaa kwenda kushuhudia pambano hilo na kusema kuwa kulikuwa na upotoshaji wa habari,

Wakati vyombo mbalimbali vya habari duniani viliporipoti pambano hilo, bondia machachari wa UFC, Conor McGregor alishangwa na maamuzi ya Mayweather na kuanza kumshambulia kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram kwakuandika maneno makali mnoo na kumzarau anayekwenda kupambana naye hali iliyopelekea Tenshin Nasukawa raia huyo wa Japan akimtaka McGregor kuwacha kumzarau na badala yake asikose kufuatilia pambano hilo na Floyd.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW