Habari

Mchizi Wangu (Remix)

Nako 2 NakoImekuwa ni historia katika gemu la muziki wa kizazi kipya hapa nchini kwa kuwepo kwa ugumu wa kuwakutanisha wasanii wenye uwezo mkubwa kisanaa na kuwafanyisha wimbo wa pamoja, lakini la kufurahisha hivi karibuni kwa mara ya kwanza wakali kibao wa muziki wa Hip Hop wameunganika na kufanya mkono wa pamoja..

Nako 2 Nako

 

Imekuwa ni historia katika gemu la muziki wa kizazi kipya hapa nchini kwa kuwepo kwa ugumu wa kuwakutanisha wasanii wenye uwezo mkubwa kisanaa na kuwafanyisha wimbo wa pamoja, lakini la kufurahisha hivi karibuni kwa mara ya kwanza wakali kibao wa muziki wa Hip Hop wameunganika na kufanya mkono wa pamoja ambao umeonekana kuwa bora kabisa kuliko ngoma zote za ushirikiano zilizowahi kufanyika.

 

Wimbo wa wasanii Nako 2 Nako ‘We ndo mchizi wangu’ hivi karibuni umerudiwa na kufanyiwa remix ambayo imewakutanisha wasanii kibao na wakali akiwemo, Jay Moe, Fid Q, Mansu-Li, Geez Mabovu, Dr K wa Mapacha, Adili Chapakazi, Chidi Benz, Mwanafalsafah, Mheshimiwa Temba, Babuu wa King’oko na wenye ngoma yao ambao ni Nako 2 Nako Souldierz.

 

Bongo5 ilipata fulsa ya kuisikiliza ngoma hiyo ambayo imerudiwa katika studio za MJ Records na Prodyuza Marco Charlie, dah ukweli kila mtu amefanya vizuri lakini wapo baadhi ya wasanii ambao wanaonekana kuhemea mipira ikiwa na maana wamejitahidi kufanya kile walichoweza japokuwa wameonekana kumezwa na baadhi yao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents