Michezo

Meddie Kagere aongoza kwa upachikaji mabao kuelekea Qatar 2022, hatua hii ya kwanza

Mshambuliaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Rwanda, Meddie Kagere ameongoza kwa kufunga mabao katika hatua ya kwanza kufuzu michuano ya kombe la dunia nchini Qatar ambayo imemamilizika.

Image result for Kagere na timu ya Rwanda

Timu ya taifa ya Rwanda imeingia hatua ya makundi kama ilivyo kwa Tanzania, ikifunga mabao 10 – 0 mbele ya Seychelles, kwenye magoli hayo nyota huyo wa Simba SC, Meddie Kagere ikifunga moja mchezo wa kwanza uliyomalizika kwa 3 – 0 na katika marudiano nchini Rwanda akipachika mawili kwenye 7 – 0 na hivyo kumfanya kuwa mabao matatu (3).

Meddie Kagere anaongoza kwa ufungaji akiwa na magoli matatu (3), akiungana na Ramadan Agab wa Suda na Joseph Mendes kutoka Guinea – Bissau.

Kwenye hatua hii ya kwanza iliyokuwa na timu 28, jumla ya mabao 57, yamefungwa katika mechi 28, hii ikiwa ni sawa na wastani wa goli 2.04 kwa kila mechi.

Hatua ya kwanza iliyokuwa na jumla ya timu 28 zenye viwango vya chini kwa mujibu wa FIFA, zilikutana na kutoa 14  Tanzania ikiwemo, ambazo sasa zitaungana na zile 26 zenye viwango vya juu zaidi ili kupata jumla ya timu 40 zitakazo ingia hatua ya makundi.

Timu zilizopita kwenye hatua hiyo ni Zimbabwe, Msumbiji, Namibia, Guinea – Bissau, Malawi, Togo, Sudan, Rwanda, Tanzania, Equitorial Guinea, Ethiopia, Liberia na Djibouti.

Jumla ya timu 14 zilizopita hatua ya kwanza na zile 26 za viwango vya juu zaidi zitafanya kuwa na jumla ni 40, ambapo zitapangwa kwenye makundi 10 yenye timu nne (4) kila moja.

Atakayefanikiwa kuongoza kwenye kundi lake atasonga mbele hatua ya tatu na ya mwisho, ambapo timu 10 hucheza za mtoano ili kupata tano (5) zitakazo iwakilisha bara la Afrika kwenye kombe la Dunia nchini Qatar 2022.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents