Membe: Afya yangu imeimarika, Sasa nipo tayari kwa kampeni za Urais naanzia Tabora

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo Bernard Membe amesema afya yake imeimarika na yupo tayari kwa ajili ya kuanza tena kampeni za Urais.

Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Bernard Membe.

Membe amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo amewaatarifu wanachama na Watanzania wote kuwa anatarajia kuwasili leo Septemba 15 nchini Tanzania kutokea Dubai.

“Afya yangu imeimarika na sasa nipo tayari kwa kampeni za Urais,  inayoanzia Tabora wiki hii hadi Oktoba 26”, amesema Bernard Membe.

“Wana ACT-Wazalendo na Watanzania wenzangu wote, Kesho Jumanne ya tarehe 15 Sept saa 8.40 mchana, nitatua Dar es salaam nikitokea Dubai”, ameongeza.

Awali Membe alizinfua kampeni zake katika Mikoa ya Lindi na Mtwara.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW