Michezo

Messi amuandikia Neymar ujumbe mzito

Kuondoka kwa Neymar katika klabu ya soka ya Barcelona kunaweza kukawa kumemuumiza zaidi Lionel Messi ambaye amekuwa karibu zaidi na mchezaji huyo kwa takribani misimu minne.

Messi kupitia mtandao wa Instagram, amemuandikia ujumbe wa kumuaga rafiki yake huyo ambaye anatarajiwa kukamilisha usajili wake wa kujiunga na PSG ya Ufaransa wiki hii kwa ada ya uhamisho utakaovunja rekodi ya dunia wa paundi milioni 198.

β€œIt was a great pleasure to have shared all these years with you, friend @neymarjr. I wish you good luck in this new stage of your life. See you tomorrow,” ameandika Messi katika mtandao huo.

Neymar alijiunga na Barca mwaka 2013 akitokea Santos ya nchini kwao Brazil.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents