Michezo

Michail Antonio: Ajifungia West Ham zaidi


Mchezaji wa West Ham, Michail Antonio

Winga, wa kikosi cha wagonga nyundo wa jiji la landani klabu ya West Ham United, Michail Antonio amesaini mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kukitumikia kikosi hiko kinashiriki Ligi Kuu nchini Uingereza.

Antonio, mwenye umri wa miaka  27 aliripotiwa kuhitajika na Viongozi wa Ligi klabu ya Chelsea, The Blues na sasa amewakata ngebe waliokuwa wakimhitaji na hatimae kuendelea kusalia katika klabu hiyo.

“Nimekuwa nikipenda kuwa hapa na ni mwenye furaha kubwa na tuna mambo mengi tumepanga,” Alisema Antonio, ambae kwa sasa ni majeruhi.

Antonio, ambae amefunga jumla ya magoli 9 katika msimu huu, aliitwa katika kikosi cha Simba watatu, timu ya taifa ya Uingereza kwa mara ya kwanza mwezi August.

Alitajwa kuwa mchezaji bora wa Msimu na klabu yake ya wagonga Nyundo wa landani, lakini hajaonekana katika Viunga vya michezo tangu mwanzoni mwa mwezi April kutokana na kukaa nje ya uwanja kwa sababu ya majeraha.


West Ham star Michail Antonio

Kutokana na uwezo wake bora ndani ya timu yake ya taifa, alikabidhiwa zawadi ndani ya kikosi hiko cha Uingereza, kwa uwezo aliouonyesha katika michezo dhidi ya Ujerumani pamoja na Lithuania mwezi March.

“Mwaka huu umekuwa bora zaidi ya mwaka jana kwasababu nimekuwa nikicheza dakika zote za mchezo na kuweza kupata nafasi katika kikosi cha timu yangu ya  taifa ya Uingereza hakika ilikuwa ndoto yangu toka utotoni,” . Alisema Mchezaji huyo wa West Ham kupitia mtandao wake.

“Nilichobakisha sasa ni kuhakikisha sishuki katika kiwango changu katika msimu mpya wa Ligi.”

Antonio, ambaye alitokea katika klabu ya Nottingham Forest Mwezi September mwaka 2015

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents