Michezo

Michuano ya Qatar Open sirafiki kwa Johanna Konta

Mchezaji tennis, Johanna Konta ameyaaga rasmi mashindano ya wazi ya Qatar Open hatua ya 16 baada ya kucheza dhidi ya Angelique Kerber.

Konta ambaye anashika nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora nchini Uingereza ametoka kwa seti 1-6 6-1 6-3 dhidi ya Kerber.

Mjerumani huyo anatarajia kukutana na Caroline Wozniacki hatua ya robo fainali.

Baada ya ushindi huo Konta ameuwambia tovuti ya  www.wtatennis.com  kuwa ilimlazimu kufika hadi raundi ya tatu ndipo kujihakikishia kupata ushindi kwakua kucheza na Johana si kitu rahisi.

“Nafikri katika raundi ya kwanza sikucheza katika kiwango na nilihitaji muda zaidi ili kuwa sawa,” Kerber aliiyambia tovuti ya www.wtatennis.com.

“Kutoka raundi ya pili ndipo nilijaribu kurejea katika kiwango na kucheza hatua kwa hatua.”

“Siku zote kunakuwa na mchezo mgumu unapokutana na Johanna, kwa kuwa ni mchezaji mzuri kwahiyo nililazimika hadi kufika raundi ya tatu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents