Habari

Mike Tyson aomba asaidiwe kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na ulevi la sivyo…..”I think of dying”

Bingwa wa zamani wa masumbwi duniani Mike ‘Iron’ Tyson amejitokeza hadharani kuomba msaada wa wasamaria wema ili aweza kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na ulevi wa pombe, na kwamba asipopata msaada huo anaweza kupotea!

Mike Tyson in The Hangover

Tyson amefunguka katika interview aliyofanya na Matt Lauer katika kipindi cha runinga kinachojulikana kama ‘Today Show’, ambapo amesema kila anapokunywa pombe na kupitiwa anawaza kuhusu kufa na kutoweka.

“When I start drinking and I relapse, I think of dying. You know I’m in a real dark mood. I think of dying and I don’t want to be around anymore. I won’t survive if I don’t get help.” Alisema

Hata hivyo Tyson ameonesha nia ya dhati ya kuachana na matumizi ya pombe na dawa za kulevya kwa kuwa ana siku 12 hajatumia dawa hizo, lakini hii inakuwa ngumu bila msaada wa ziada.

Mkali huyo wa ndondi aliyekuwa gumzo enzi hizo, amesema anajutia maisha anayoyapitia na kwamba hakuna mtu aliyefeli na kupitia maumivu makali kama aliyopitia yeye, lakini sasa anataka kuwa mtu wa kawaida na kubadili kabisa maisha yake, anasisitiza “I don’t wanna Die.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents