BurudaniHabari

Miss Temeke 2006 asaidia yatima Keko

MNYANGE aliyeshika nafasi ya pili Miss Tanzania 2006, Jokate Mwegelo ametoa msaada wa sh. 200,000 katika kituo cha watoto yatima cha Mkombozi kilichopo Keko Machungwa, Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wa Majira

MNYANGE aliyeshika nafasi ya pili Miss Tanzania 2006, Jokate Mwegelo ametoa msaada wa sh. 200,000 katika kituo cha watoto yatima cha Mkombozi kilichopo Keko Machungwa, Dar es Salaam.

Jokate ambaye pia ni Miss Temeke 2006 anayeshikilia taji la mlimbwende wa Redd’s, alikabidhi msaada huo katika hafla iliyofanyika kituoni hapo, jana.

Jokate alisema msaada huo ni sehemu ya ahadi aliyoitoa alipotembelea kituo hicho kugawa vyeti kwa watoto waliohitimu elimu ya awali Desemba mwaka jana.

Alisema kwa kufahamu umuhimu wa elimu kwa watoto, ameona ni vyema akatoa msaada huo utakaosaidia kununulia vfifaa vya masomo na malezi ya watoto wanaolelewa kituonmi hapo.

Aliwataka watu mbalimbali wenye uwezo ikiwa ni pamoja na kampuni na mashirika kujitokeza kuwasaidia watoto waliopo katika vituo mbalimbali kwa vile ndio njia pekee ya kuwaonesha watoto kuwa jamii inawajali.

Mkuu wa kituo hicho, Michael Maurus, alimshukuru mnyange huyo na kuwataka wengine kuiga mfano wake badala ya kujihusisha katika matendo yanayoharibu sifa za urembo wao.

Alisema kituo chake kina watoto yatima sita na wasio yatima 59 na kwamba walio yatima wamekuwa wakilelewa kituoni hapo bila kutegemea msaada kutoka kwa yeyote zaidi ya michango kidogo inayotolewa na wazazi wa watoto wasio yatima.

Aliahidi kuutumia msaada huo kununulia vifaa vya masomo kwa watoto wote ikiwa ni pamoja na sare kwa yatima waliopo kituoni hapo.

Source: Majira

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents