BurudaniHabari

Kumbi 23 za starehe kushitakiwa

WAMILIKI 23 wa kumbi za starehe katika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wako kwenye hatihati ya kuburuzwa mahakamani na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA)

na Agnes Mlundachuma

 

WAMILIKI 23 wa kumbi za starehe katika Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, wako kwenye hatihati ya kuburuzwa mahakamani na Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA), kwa kushindwa kulipia kazi za wasanii mbalimbali wanazozitumia katika maeneo yao ya biashara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi, Ofisa Leseni wa COSOTA, Yustus Mkinga, alisema wamiliki hao waliogoma kulipa, ni watumiaji wakubwa wa kazi hizo.

Ofisa huyo alisema, wamiliki hao wanatakiwa kulipa fedha hizo kwa kufuata kanuni ya utoaji leseni za uonyeshaji na utangazaji wa kazi za sanaa katika sehemu za biashara ya mwaka 2003.

Alisema, kuburuzwa kwa wamiliki hao ni mwanzo tu, kwani kazi hiyo itaendelea katika mikoa yote.

Mkinga alisema, kwa mwaka jana, wamefanikiwa kukusanya sh milioni 80 nchi nzima ambazo zitaenda kwa wasanii husika.

Aliongeza kuwa, hivi sasa COSOTA ipo katika mchakato kuwasiliana na wamiliki wa vituo vya redio na televisheni ili nao waanze kulipia kazi za wasanii wanazozitumia.

Mkinga alisema, kiwango cha chini kitakachokuwa kikilipwa na wamiliki hao ni sh 500,000 kwa matumizi ya kawaida kwa redio na televisheni, lakini iwapo kituo kitakuwa na matumizi makubwa zaidi kitapanda.

 

Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents