Aisee DSTV!

‘Mission’ ya Juventus kumnasa meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri baada ya fainali ya Europa League hii hapa, muda pekee ndiyo unao subiriwa

Kocha asiye na maneno mengi ndani ya ligi kuu England na mpenzi mkubwa wa kutumia sigara kama sehemu ya kiburudisho chake, Maurizio Sarri ameendelea kuwa chaguo kubwa la vibibi vya turin klabu ya Juventus huku miamba hiyo ya soka ya Italia ikitarajia kumpatia kandarasi mara baada ya fainali za Europa League.

Maurizio Sarri remains 'favourite' in the eyes of Juventus as they eye their next manager

Sarri kwa sasa anakiandaa kikosi chake kuikabili Arsenal huko Baku kunako Mei 29 huku akiwa hana uhakika na maisha yake ndani Stamford Bridge licha ya kuiweka The Blues katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi hiyo na kuwa kwenye uwezekano wa kutwaa taji kubwa la Europa League.

The front page of Gazzetta dello Sport on Friday shows the Chelsea boss linked with Juventus

Mbele ya gazeti la michezo la Gazzetta dello Sport lililotoka hii leo siku ya Ijumaa limemuhusisha kocha huyo wa Chelsea na Juventus

Ukiachia mbali Sarri, klabu ya Juventus pia imeonyesha nia ya yakumtaka kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino lakini mipango hiyo inaonekana kuwa migumu kutokana na Muargenta huyo kuwa na kandarasi na timu hiyo ya London Kaskazini.

Manchester City boss Pep Guardiola is also of interest but Sarri is seen as an attainable target

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola pia amehusishwa lakini Sarri ameonekana kuwa ndiyo tageti kubwa ya miamba hiyo ya soka kutoka Italia.

Bosi huyo wa zamani wa Napoli, ametokea kwenye kurasa za mbele za gazeti la michezo la Ijuma hii  La Gazzetta dello Sport kutoka Italia na kuripotiwa kuwa Sarri alikuwa kwenye kikao cha siri na Mkurugenzi wa timu ya Juventus, Fabio Paratici.

Hata hivyo, Paratici alifanya ziara yake hadi jijini London kukutana na kaka wa kocha wa Spurs, Pochettino ambaye inadaiwa kuwa ndiye wakala wake ambao wote hawa wanatazamiwa kuchukua mikoba ya Allegri.

Sarri anawavutia Juventus kutokana na uwajibikaji wake kwa maendeleo ya wachezaji na aina ya mfumo wake wa uchezaji.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW