Michezo

Mlindalango, Gianluigi Buffon amjia juu mwamuzi, Michael Oliver kwa kuipa Real Madrid penati (+Picha)

Mlindalango wa klabu ya Juvetus, Gianluigi Buffon amesema kuwa mwamuzi wa mchezo wao dhidi ya Real Madrid, Michael Oliver ndiyo muuwaji wa ndoto za timu yao hapo jana kwa kuruhusu adhabu ya penati ambayo kwa upande wake aliona haikuwa sahihi.

Buffon, alimjia juu mwamuzi, Michael Oliver kutoka Uingereza kwa kuruhusu penati ambayo haikuwa sahihi kwa upande wake dakika za nyongeza kabla ya mchezo huo kuisha baada ya mshambuliaji wa Madrid, Lucas Vazquez  kusukumwa eneo la penati boksi na kuamuriwa hadhabu hiyo iliyo fanya mchezo huo kumalizika kwa matokeo ya jumla ya mabao 3 – 1 na vijana wa Hispania kusonga mbele hatua ya nusu fainali kwa jumla ya magoli 4-3 wakati huo huo kipa huyo mkongwe akipata kadi nyekundu.

Gianluigi Buffon ameyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo ambao huwenda ukawa wa mwisho kwake kufuatia kuamua kustaafu soka la kulipwa.

Mwamuzi, Michael Oliver kwenye kifua chake hana roho ya huruma hata chembe, alikuwa muuwaji wa ndoto za Juventus anachoweza yeye ni kukaa na familia yake na kunywa Sprite na kula ‘crisps’ tu.

Katika mchezo mwigine uliyopigwa uwanja wa Allianz Arena, Bayern Munich imesonga mbele mpaka hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1 dhidi Sevilla baada ya hapo jana kutoka sare ya 0 – 0.

Picha za matukio mbalimbali ya uwanjani kwenye mchezo wa Real Madrid dhidi ya Juventus ambao ulimalizika kwa mabao 3 – 1.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents