Michezo

Mnyama Simba aendeleza ubabe nje ya Uwanja, aweka rekodi zake sawa ”Tupo mbali sana”

Mabingwa wa tetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC, imeandika rekodi kwa kuwa klabu ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na wafuasi wengi zaidi kupitia akaunti yake ya kijamii ya Instagram.

Mapema jana usiku miamba hiyo ya soka ya Tanzania Bara ili fikisha jumla ya idadi ya wafuasi Milioni moja hii ni kwa mara ya kwanza kwa klabu zinazopatika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati kufikia kiasi hiko.

Kwa upande wao Simba, imeyapokea matokeo hayo kwa furaha kubwa na kuwashukuru wapenzi na mashabiki wake.

”Wafuasi milioni moja (1,000,000) kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Afrika Mashariki na Kati tumekuwa timu ya kwanza kufikisha idadi hiyo. Asanteni Wanasimba wote na watu wote ambao wamezifuata kurasa za mabingwa wa nchi. Tupo mbali sana,” Imeandika Simba SC

Hapa nchini timu kubwa ambazo zina wafuasi wengi ukiachana na Simba ni Yanga na Azam FC.

Yanga SC ina wafuasi 429K

Azam FC ina wafuasi 246K

Mtibwa Sugar ina wafuasi 133K

Mbeya City ina wafuasi 85.5K

KMC FC ina wafuasi 103K

Ukiachana na hizo kwa hapa nyumani zipo timu kubwa mbili ambzo nazo zinatikisa soka la Afrika Mashariki nazo ni Gor Mahia

Gor Mahia ina wafuasi 29.7 K

AFC Leopards ina wafuasi elfu 4545.

Pale Uganda kuna timu kama URA FC ambayo yenyewe ina wafuasi 1064 .

Mbali na hiyo, Mnyama Simba mapema hivi karibuni aliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kutinga hatua ya robo fainali ya Michuano ya klabu bingwa Barani Afrika.

Ikumbukwe kuwa Simba ndiye bingwa mtetezi wa kombe la ligi kuu soka Tanzania Bara kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kufanikiwa kulinyakuwa katika awamu mbili zilizopita na mpaka sasa amekuwa hakamatiki kwenye msimamo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents