Michezo

Mohamed Salah kustaafu soka la kimataifa, ahusishwa kuamia Urusi

Baada ya maneno mengi yanayo muhusu mshambuliaji hatari wa Misri, Mohamed Salah kutaka kustaafu soka la kimataifa mara baada ya mchezo wake wa mwisho dhidi ya Saudi Arabia, Chama cha soka cha mafarao hao FA  kimesema kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika mpaka sasa dhidi ya mchezaji huyo.

Inaelezwa kuwa mshambuliaji huyo wa klabu ya  Liverpool ya nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 26, hana mahusiano mazuri na chama cha soka nchini Misri FA hivyo kustaafu baaada ya mchezo wake wa leo.

Habari hizo zimezidi kuenea kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kiongozi wa Chechnia, Ramzan Kadyrov kumtangaza kumpatia uraia wa heshima wa Urusi mshambuliaji huyo, Mohamed Salah

Mohamed Salah akiwa na kiongozi wa Chechnia, Ramzan Kadyrov 

Hatua ya Kadyrov imekosolewa vikali huku akishutumiwa kumtumia Salah kwa propaganda zake za kisiasa huku wengine wakiamini kuwa ni kweli mchezaji huyo atatoa mkono wa kwa heri hii leo.

Hatakama chama cha soka nchini Misri kimesema kustaafu kwake hakuna umuhimu wowote kwao bado wamesisitiza kuwa wanafanya mazungumzo na mchezaji huyo.

“Tumetumia siku nzima tukiwa naye na kamwe hatukuzungumza naye kuhusu swala hili. Tupo hapa Urusi kwaajili ya michezo na tunafuata kanuni na sheria za FIFA hatuwezi kuzungumzia siasa na kama kutakuwa na maswala kama hayo ya siasa tungeelezwa na FIFA.” Limesema shirikisho hilo la Misri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents