DStv Inogilee!

Monalisa na Bofeda uso kwa uso Marekani

Msanii wa filamu Bongo, Monalisa atakutana na staa filamu kutoka Nigeria (Nollywood), Bofeda Moji nchini Marekani.

Wawili hao na wasanii wengine kutoka Afrika watakutana Dallas Marekani kuanzia June 29 hadi July 03, 2018 katika Tamasha la filamu ‘The African Film Festival’ ambalo Bofeda ndiye host.

Katika Tamasha hilo Monalisa atakutana na mastaa wengine kama Naomi Achu kutoka Cameroon, Kelechi Eke kutoka Nigeria na wengineo. Monalisa ndiye msanii pekee atakayeiwakilisha Tanzania katika tamasha hilo.

Utakumbuka April 14, 2016 Monalisa alishinda tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika. Tuzo hizo zilitolewa Accra nchini Ghana, Msani mwingine wa Tanzania aliyeshinda katika tuzo hizo ni Ray Kigosi.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW