Mourinho awalinganisha Barcelona na watoto wadogo U14, baada ya kipigo dhidi ya Liverpool ‘Watoto wamelala/ ni kitu kigumu kwangu kuelezea’
“Kama unaangalia bao lile kwa watoto wa chini ya umri wa miaka 14 au 15 ungeweza kusema, watoto wamelala, watoto hawapo sawa kiakili kucheza mpira, watoto wanahitaji kujifunza zaidi kuhusiana na msingi wa mechi.” Mourinho ameiyambia beIN SPORTS.
Jose Mourinho ameongeza “Lakini tunazungumzia wachezaji bora kabisa ulimwenguni, bao ambalo hukuonyesha kwamba hakukuwa sawa kiakili.”
“Katika kipindi cha mapumziko nilisema kama Liverpool watafunga bao la pili basi hali ya uwanja itabadilika, na hakika yakibadilika yatakuwa mazingira magumu sana kwenda nayo sawa.”
“Lakini Barcelona wanabaadhi ya wachezaji bora kabisa ulimwenguni. wenyewe asili yao ni kucheza levo ile ile. asili yao kucheza dhidi ya Real Madrid, kuingia fainali, nusu fainali ya Champions League final kila msimu kwao ni kitu cha kawaida.”
“Ni kitu kigumu sana kwangu kukielezea, ni vigumu sana kuamini kwamba timu yangu imeshinda mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza alafu nakuja kupoteza 4-0 mechi ya marudiano. Ningelipenda kuona Valverde akijaribu kuelezea lakini naamini itamuwia ugumu kwake kuzungumzia.”
Kwa matokeo hayo ya jumla ya mabao 4 – 3, Liverpool sasa inasubiria mshindi kati ya timu ya Ajax au Tottenham ili kucheza kwenye hatua ya fainali ya michuano hiyo mikubwa barani Ulaya.
Mourinho amewahi kuikabili mara kadhaa Barca wakati akiwa kocha Mkuu wa Real Madrid mwaka 2010 hadi 2013.