Michezo

Mourinho kutafuta mbadala wa Michael Carrick

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa kunahaja ya kusajili kiungo mwingine kipindi cha majira ya joto atakae rithi mikoba ya Michael Carrick.

Carrick mwenye umri wa miaka, 36 anatarajia kustaafu soka na kujiunga na benchi la ufundi la Mourinho mwishoni mwa msimu huu huku akihitimisha safari yake ya miaka 12 ndani ya Old Trafford baada ya kujiunga mwaka 2006 akitokea Tottenham Hotspur.

Alipoulizwa na waandhishi kama atampandisha kijana kuchukua nafasi ya mchezaji huyo wakati wa dirisha la usajili Mourinho amesema “Tunahitaji kusajili nafasi ya kiungo kwa sababu tunaelekea kumpoteza Michael Carrick,”amesema Mourinho.

Mourinho amewaambia waandishi wa habari “Wakati si hitaji kuzungumza kitu jua sihitaji, lakini sihitaji kukupeleka katika muelekeo mwingine.”

“Kwa hiyo nawaambia hatuhitaji kusajili mshambuli yoyote ama winga na ndiyomaana nikasema tunahitaji kiungo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents