Michezo

Mpira umri, Fernando Torres kumalizia maisha ya soka nchini Japan (+Picha)

Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid na Liverpool, Fernando Torres ameamua kwenda kumalizia maisha yake ya soka nchini Japan.

Nyota huyo wa Hispania, Torres mwenye umri wa miaka 34 amethibitisha kutarajia kujiunga na klabu ya Sagan Tosu ya nchini Japan msimu ujao.

Baada ya kuhusishwa na kutimkia Marekani au Australia hatimaye kupitia mkutano na waandishi wa habari leo siku ya Jumanne majira ya hasubuhi amethibitisha kuelekea bara la Asia ambapo atajiunga na rafiki yake Andres Iniesta nchini Japan.

Kuelekea kwake ligi ya Japan kunadhihirisha kuwa umri wake umekwenda na hivyo hawezi kucheza kwenye klabu zenye ushindani mkubwa na ndoto za kuyafikia mafanikio makubwa na hii wala siyo yeye wa kwanza wapo wakina Wayne Rooney, Andres Iniesta na wengine ambao wametimkia China kumalizia maisha yao ya soka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents