Michezo

Mrisho Ngasa ‘Uncle’ aibeba Yanga mbele ya Azam FC, wazidi kujikita kileleni mwa ligi

Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga hii leo imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya waoka mikate Azam FC mchezo uliyopigwa kwenye uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Vinara hao wa ligi kuu Yanga SC wamepata bao lao dakika ya 13 kupitia kwa nyota wake Mrisho Ngasa.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuzidi kujikita kileleni mwa ligi hiyo kwa kuwa na jumla ya pointi 77, Azam FC ikisalia na alama zake 66 kwakuwa nafasi ya tatu zote zikiwa zimeshacheza jumla ya michezo 33.

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya ushindi wao wa hapo jana wamejikusanyia jumla ya pointi 69 wakiwa nafasi ya pili kwa kucheza jumla ya mechi 27.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents