Michezo

Mrisho Ngassa ajichora tattoo ya jina la mkewe

Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa jana April 21 katika mechi dhidi ya Stand United iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam alifunga goli moja lakini hakushangilia kwa kawaida yake ya kwenda kwenye kona ya kibendera, bali alionekana akibusu mkono wake.

20150421_182508

Ngassa aliongea na kipindi cha Sports Xtra cha Clouds FM na kueleza kwanini aliubusu mkono wake.

“Nimebusu mkono kwasabababu nimechora ‘Tattoo’ ya jina la mke wangu. Mke wangu ndio kila kitu, ndio mshauri wangu wa kila kitu, kwahiyo nikifunga goli lazima nimbusu,” alisema.

“Tattoo niliyochora ni jina la mke wangu kwasababu nina mapenzi ya dhati kwake, yeye ndiye mshauri wangu, anaitwa Nish Radhia. Kuna tattoo nyingine ambayo ni siri yangu pamoja na yeye, imechorwa kifuani.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents