Michezo

Msimamo wa makundi ya UEFA Champions League

Michezo kadhaa ya klabu bingwa barani Ulaya ilipigwa usiku wa jana, Liverpool walitoka sare ya mabao 3 kwa 3 dhidi Sevilla, Real Madrid nao wakifunga jumla ya mabao 6 kwa bila na Apoel.

Manchester City wakiendeleza makali yao baada ya kutoka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Feyenoord, wakati Tottenham nao wakiibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Dortmund.

Na huu ndiyomsimamo wa makundi unavyoonyesha baada ya michezo ya hapojana siku ya Jumanne kumalizika.

Kundi A, linaongozwa na Manchester United yenye alama 12, ikifuatiwa na FC Basel yenye pointi 6 na nafasi ya tatu ikishikwa na CSKA Moscow yenye alama 6.

Kundi B, linaongozwa na Paris Saint Germain wenye alama 12, ikifuatiwa na Bayern Munich wakiwa na alama 9 na nafasi ya tatu ikishikwa na Celtic wakiwa na pointi 3.

Kund C, ikiongozwa na Roma wenye alama 8, ikifuatiwa na Chelsea wenye pointi 7 na nafasi ya tatu ikishikwa na Atletico Madrid wakiwa wamejikusanyia alama 3.

Kundi D, linaongozwa na Barcelona kwakuwa na alama 10, nafasi ya pili ikishikwa na Juventus wenye pointi 7 na ya tatu wakishika Sporting Lisbon wenye alama 4.

Kundi E, Liverpool inaongoza kwa kuwa na alama 9, ikifuatiwa na Sevilla wenye pointi 8 na watatu katika kundi hilo ni timu ya Spartak Mosco wenye alama 6.

Kundi F, Manchester City inaongoza kwa kuwa na alama 15 ikifuatiwa na Shakhtar Donetsk wenye point 9 na ya tatu ni Napoli ikiwa na alama 6.

Kundi G, Besiktas inaongoza kwa kuwa na alama 11, nafasi ya pili ikishikiliwa na FC Porto wenye pointi 7 na ya tatu ni RB Leipzing wakiwa na alama 7.

Kundi la mwisho ni H, likiongozwa na Totteham Hotspur wakiwa na pointi 13, Real Madri alama 10 na Borussia Dortmund wenye pointi 2.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents