Michezo

Mtabiri maarufu mjini Sumbawanga aipa Simba ushindi ‘Mvua itanyesha Dar wiki nzima, Yanga isipofunga dakika 45 za kwanza imekwisha’

Kuelekea mchezo wa watani wa jadi Simba SC dhidi ya Yanga hapo kesho siku ya Jumapili uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mtabiri maarufu wa mechi mbalimbali kutoka mjini Sumbawanga, Isaya Germano maarufu kama Dkt Kataushanga ameitabiria makubwa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba mbele ya watani wao wa Jangwani.

Kupitia mahojiano yake na kituo cha Azam Tv, Dkt Kataushanga amesema kuwa mvua itaendelea kunyesha jijini Dar es salaam kwa muda mfupimfupi kwa wiki nzima hadi kwenye mchezo wa Simba na Yanga utakao pigwa hapo kesho Septemba 30.

Pamoja na mvua kunyesha Dkt Kataushanga ametabiri Simba itaibuka na ushindi kwenye mchezo huo huku akisisitiza kuwa ushindi wa Yanga ni sare tu na si vinginevyo.

”Mechi naiyona kwa mtazamo tofauti aina tatu, moja ni kila timu kiwango chake Simba inauwezo wa kucheza dakika 90, Yanga inacheza dakika 45 kwa hiyo Simba akijitahidi asifungwe na Yanga kipindi cha kwanza Yanga ameondoka,” amesema Dkt Kataushanga.

Dkt Kataushanga ameongeza kuwa ”Kwa kadri michezo iliyochezwa bila vitu vingine vyovyote Simba anamfunga Yanga, upepo unatoka hapa unapeleka mawingu Dar es salaam alafu mvua inanyesha huko lakini upepo unachezwa wapi Sumbawanga.”

”Leo mvua imenyesha dakika 15 Dar es salaam alafu upepo unapiga wapi Sumbawanga, sasa inanielezaje hiyo maana yake ni nini ?  je ni magoli ?, nani anayefungwa ? kwanza mpira unachezwa Jumapili kwa nyota tu Simba imekaa yani upende usipende ni nyota yake.”

Simba na Yanga ni mchezo namba 72 ambao unatarajiwa kupigwa saa 11 jioni hapo kesho huku Serikali ikihamasisha hali ya usalama kutokana na ukubwa wake wakati mashabiki wa soka wakitarajiwa kufurika uwanjani siku hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents