Technology

Mtandao mpya wa simu ‘Smart Telecom’ wazinduliwa Dar es Salaam

Mtandao mpya wa mawasiliano ya simu ‘Smart Telecom’ umezinduliwa leo jijini Dar es salaam katika Hotel ya Serena ambapo msanii wa vichekesho nchini Hemed Maliyaga maarufu kwa jina la Mkwere amechukua nafasi ya ubalozi hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart East Africa, abellatif bouzian (kushoto) akizungumza jambo
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart East Africa, abellatif bouzian akizungumza

Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji mkuu wa Smart Telecom, Abdellatif Bouziani amesema mtandao huo ulipewa jina na Wanaafrika Mashariki baada ya kuandaa mchakato wa uliyoitwa ‘Give us a Name’

“The name Smart was chosen as the name by the people of East Africa in an innovative naming campaign, ‘Give us a Name’, Smart Telecom is under Industrial Promotion Services (IPS) Kenya, a subsidiary of the Aga Khan Fund for Economic Development (AKFED),”alisema Abdellatif Bouziani

Bouziani alisema mtandao wa Smart Mobile umeanza na unatoa huduma hapa nchini kwa kiwango cha chini ambacho kinalingana maisha ya Mtanzania mwenye maisha ya kawaida.

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart East Africa, abellatif bouzian (kushoto)   na katikati ni Hemed Maliyaga aka Mkwere ambae ni balozi wa Smart Mobili wakiwa na mdau wao
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart East Africa, Abellatif Bouzian (kushoto) na katikati ni Hemed Maliyaga aka Mkwere ambae ni balozi wa Smart Telecom wakiwa na mdau wao

Katika hatua nyingine balozi wa mtandao huo hapa nchini mchekeshaji, Mkwere amesema mtandao huo utawawezesha wananchi kuwasiliana kwa bei ya chini kulingana na maisha halisi.

“Kwanza leo nimefurahi kukutana na mabosi wangu na pia napenda kuwaambia Watanzania wenzangu wajiunge na mtandao wa Smart Telecom ambao una huduma za chini kulingana na kipato cha Mtanzania. Kwahiyo mimi kama balozi wenu nimefurahia kuona kuna mtandao ulioanzishwa kwaajili ya kuhudumia watu wetu.”

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart East Africa, abellatif abouzian akimkabidhi mdau zawadi
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Smart East Africa, Abellatif Abouzian akimkabidhi mdau zawadi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents