Michezo

Mtibwa Sugar yakutana na kigingi kizito, yatakiwa kulipa mamilioni kushiriki michuano ya CAF

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu wake, Wilfred Kidao limesema kuwa klabu ya Mtibwa Sugar italazimika kulipa dola za Kimarekani 1500 kama itahitaji kushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Mtibwa watalazimika kulipa gharama zote za safari zilizotumiwa na wapinzani wao klabu ya Santos ya Afrika Kusini kabla haijafika Julai 20 mwaka huu 2018.
Gharama zote hizi zinaikabili klabu ya Mtibwa Sugar baada ya kufungiwa miaka mitatu ya kutoshiriki mashindano yoyote kutoka Shirikisho la soka Afriaka CAF baada ya kushindwa kupeleka timu Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wake na Santos.
Kidao, amesema Mtibwa inapaswa kuwajibika katika gharama hizo za klabu ya Santos pamoja na faini hiyo iliyotlewana na CAF ili Iweze kupata nafasi ya ushiriki wa mashindano hayo.
Mtibwa Sugar ilipata nafasi ya kushiriki mashindano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kuifunga timu ya Singida United kwenye mchezo wa fainali ya FA kwa jumla ya mabao 3 – 2 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents