Habari

Mtoto wa kiume azaliwa na vichwa viwili katika mwili mmoja huko India, madaktari wasema wanaamini wanaweza kumuokoa

Watoto mapacha wa kiume wamezaliwa huko India wakiwa na vichwa viwili katika mwili mmoja kitu ambacho inasemekana ni nadra sana kutokea.

twin-2

Madaktari wamesema wanaamini wanauwezo wa kuokoa maisha ya watoto hao ambao wamezaliwa Jumatano (July 24) huko Jaipur, Rajasthan India.

Kwa mujibu wa taarifa ya Daily Mail, nervous system ya watoto hao imetengana wakati uti wa mgongo umeungana na pia wanashare sehemu ya ubavu.

twin-1

Dr. S.D. Sharma, wa J.K. Lone Hospital amesema tatizo kama hilo ni nadra sana kutokea hususan kwa watoto wa kiume, na linafahamika kama ‘Dicephalic Parapagus’. Aliongeza kuwa tukio hilo ni la pili kutokea India.

Daktari huyo aliendelea kusema kuwa mara nyingi watoto wenye ‘Dicephalic Parapagus’ huzaliwa wakiwa wamekufa, na mara nyingi hutokea kwa watoto wa kike. Kwa mujibu wa Sharma alisema kuna uwezekano wa kuokoa maisha ya mapacha hao.

twin-3

Tatizo kama hilo lililowahi kutokea kwa mapacha wa kike kutoka Sudan mwaka (2011) ambao waliozaliwa wakiwa wameungana vichwa. Watoto hao Rital na Ritag Gaboura walifanikiwa kutenganishwa salama japo kwa tatizo kama lao uwezekano wa kupona hua ni kwa mmoja kati ya million kumi.

twin-4
Rital na Ritag Gaboura wa Sudan baada ya kutenganishwa

Inasemekana tatizo la mapacha kuzaliwa wameungana hutokea mara moja kati ya watoto 100,000 wanaozaliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents