Habari

Mtu mmoja akamatwa baada ya kukutwa juu ya paa la nyumba ya Rihanna usiku

Mwanaume mmoja mwenye miaka 26 amekamatwa na kufikishwa polisi baada ya walinzi binafsi kumkuta juu ya paa la nyumba ya mwimbaji wa ‘Diamonds’ Rihanna ambaye hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo.

Ri

Walinzi wa eneo hilo wamedai kuwa walimwona mtu huyo juu ya paa la nyumba ya mwimbaji huyo iliyoko Pacific Palisades, Los Angeles nchini Marekani jana (June 18) saa 4 usiku na kumkamata. Baada ya kumweka chini ya ulinzi waliwapigia simu polisi ambao walikuja kumchukua mtu huyo ambaye mpaka sasa amewekwa ndani.

Rihanna ambaye yuko katika Diamonds World Tour hakuwepo nyumbani kwake wakati wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa TMZ mtu huyo alidai kuwa hakujua kama hiyo ni nyumba ya Rihanna lakini polisi wa eneo hilo walisema mtu huyo alikuwa na Google Map ya eneo hilo katika display ya simu yake wakati anakamatwa.

Tukio lingine la kufanana na hili katika makazi ya Riri lilitokea mwezi (February) mwaka huu baada ya walinzi kumkamata mtu mwingine aliyeingia katika nyumba ya jirani wa Rihanna akijua ni ya Riri. Mtu huyo aliiba baadhi ya vitu na kisha kulala kwenye kitanda cha moja ya vyumba vya nyumba hiyo akidhani ni kitanda cha Rihanna!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents