Habari

MultiChoice yaungana na UN kwenye kampeni maalum ya COVID-19

MultiChoice yaungana na UN kwenye kampeni maalum ya COVID-19

Kundi la makampuni ya MultiChoice limetangaza mkakati wao mpya wa kusaidia katika kupambana na janga la COVID19 kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) ambapo wamezindua kampeni maalum ya kukabiliana na usambazaji wataarifa zisizo sahihi kwa umma.

Kampeni hiyo imezinduliwa kwa kuzingatia ukweli kuwa kumekuwa na taarifa zisizo sahihi na ambazo hazitoki katika vyanzo na mamlaka husika na maranyingi taarifa hizo huleta taharuki, woga na hofu kwa umma na hivyo kuathiri jitihada za kupambana na janga la COVID-19 kote duniani.

Tangu kulipuka kwa ugonjwa huo, MultiChoice imekuwa mstari wa mbele katika kupambana ambapo ilianza kutumia vyombo vyake kutoa matangazo ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya vifaa muhimu vya kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika muendelezo huo, sasa MultiChoice imeungana na umoja wa mataifa kwenye kampeni mahsusi ijulikanayo kama ‘Pause’ ambayo inawaasa watu kuacha kutunga au kusambaza habari zisizo thibitiswa na mamlaka stahiki kuhusu COVID-19 kwakuwa habari hizo zinaleta madhara kwa umma.

Mwenyekiti Mtendaji wa kundi la makampuni ya MultiChoice Imtiaz Patel, amesema “Tuko katika wakati mgumu ambapo tunashuhudia madhara mbalimbali ya kiuchumi na kijamii yanayosababishwa na mlipuko wa COVID-19. Katika kipindi hiki, habari zisizo sahihi, zenye kupotosha na zauvumi zimekuwa kikwazo kikubwa katika kupambana na janga hili hivyo tumeona tuungane na Umoja wa Mataifa katika kampeni hii mahsusi ya kushawishi watu kuacha kusambaza, kubuni na kuzusha taarifa zozote zile zisizo thibitishwa kuhusu maradhi haya”

Imtiaz ameongeza kuwa “Utoaji na usambazaji wa habari sahihi kutoka kwenye vyanzo sahihi na mamlaka husika ni muhumu sana katika kupambana na ugonjwa huu na ndiyo sababu MultiChoice imeamua kuungana na Umoja wa Mataifa ili kuruhusu vyombo vya habari kushiriki katika kampeni hii muhimu.”

Kuifuatiliakampenihiitembelea#TakeCareBeforeYouShare

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents