Michezo

Muogeleaji awaokoa wapenzi waliokuwa hatarini kuzama

Muogeleaji wa Italia Filippo Magnini amemuokoa Anrea Benedetto ambaye alikuwa akizama kwenye maji siku ya Jumapili.

Filippo Magnini, picha ya 2009

Bingwa wa zamani wa michuano ya kuogelea alijitosa majini baada ya marafiki wa mwanaume huyo kuanza kupiga kelele katika ufukwe wa Cala Sinzias.

Magnini aliunyanyua uso wa Benedetto juu ya maji mpaka wahudumu waokoaji walipowasili.

”Nilianya nilichotakiwa kufanya,” mwanamichezo huyo mstaafu alisema.

Ni siku mbili pekee kabla, bwana Benedetto, 45, alikua amefunga ndoa na mpenzi wake wa jinsia moja.

Tukio hilo la Jumapili lilishuhudiwa na rafiki wa wapenzi hao na mwandishi wa habari wa eneo la uajemi, Soroush Paksad.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Wapenzi hao walikuwa wakielea wakiwa juu ya boya, kabla ya Benedetto kuangukia kwenye maji, yaliyokuwa yabaridi kuliko ilivyotarajiwa, hivyo hakuweza kusogeza miguu yake kutokana na hali ya kiafya.Andrea Benedetto

Kelele za marafiki zake kuomba msaada zilisikiwa na wafanyakazi waokoaji, ambao waliharakisha kwenda kumuokoa.

Lakini muogeleaji Magnini alikuwa karibu wakati huo hivyo aliharakisha na kumfikia Benedetto.

” Alikuwa akisumbuka sana: alikuwa akiogopa, pia alikunywa maji, ”Magnini alieleza.

Allan Buberwa: Mwanafunzi wa kitanzania aliyefia mtoni Marekani azikwa Dar es salaam

”Nilipomfikia hakuweza hata kuzungumza, na haikuwa rahisi kumnyanyua, hivyo tulimlaza kwenye boya la kitanda walilokuwa nalo waogaji wengine.

”Nilipopata fahamu jambo la kwanza kulifikiria lilikuwa mume wangu,”alieleza.

”Saa chache baada ya ajali nilikuwa hospitalini ndipo nilipogundua kuwa Filippo Magnini ndiye aliyemuokoa lakini sikupata muda wa kumshukuru kwa kuwa sikuwa na mawasiliano.Nina matumaini nitaweza kumshukuru mimi binafsi.”

Giorgia Palmas na Filippo Magnini, 2018Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Magnini alikuwa ufukweni na mpenziwe Giorgia Palmas, mwanamitindo na mtangazaji wa televisheni.

Magnini aliwahi kushinda medali ya shaba mwaka 2004 aliposhiriki michuano ya kuogelea kwa mitindo huru, michuano ya Olimpiki mjini Athens.

Pia alikuwa mshindi wa dunia mita 100 mitindo huru mwaka 2005, na kulitetea taji lake mwaka 2007.

Utajuaje kuwa mtu anataka kuzama

  • Mtu aliye hatarini kuzama kiaikolojia hushindwa kuomba msaada. mfumo wa upumuaji upo kwa ajili ya kupumua, hivyo kuzungumza si jambo la msingi.
  • Midomo ya watu wanaozama huzama kisha hujitokeza juu ya uso wa maji. Midomo hushindwa kuwa juu ya uso wa maji kwa muda mrefu kuwezesha watu kuomba msaada, huvuta pumzi na kuziachia haraka sana wakati wanaanza kuzama.
  • Hawawezi kupunga mkono kuomba msaada.
  • Hutapatapa juu ya uso wa maji kwa sekunde 20-60 kabla ya kuzama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents