Michezo

Mvua yawaokoa waarabu, Mnyama Simba SC atoka na uchu

Vinara wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Simba hii leo imelatoka sare ya mabao 2 – 2 dhidi ya timu ya Al-Misry ya nchini Misri katika mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Katika mchezo huo uliyokuwa na ushindani wa hali ya juu kwa pande zote mbili waliyoanza kupata bao walikuwa ni Simba SC kupitia kwa mshambuliaji wake hatari, John Bocco dakika ya 10 kisha mchezaji wa Al-Masry, Ahmed akaisawazishia dakika ya 11 na kisha kupata la pili kupitia kwa Abdalrauf dakika ya 26 na Emmanuel Okwi akaisawazishia bao hilo la pili dakika ya 74 na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare hiyo ya mabao 2 – 2.

Hata hivyo mchezo huo ulisimama kwa saa kadhaa kufuatia kuzimika kwa taa za uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kisha mvua kubwa kunyesha hali iliyopelekea baadhi ya wachezaji na waamuzi wa mchezo huo kuoondoka ndani ya uwanja hii ikitokea baada ya dakika chache tu toka mshambuliaji wa Simba SC raia wa Uganda, Emmanuel Okwi kuipatia timu yake bao la kusawazisha.

Simba SC sasa italazimika kushinda jumla ya mabao 2 – 0 dhidi ya Al-Masry huko nchini Misry ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele na michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents