Moto Hauzimwi

Mvulana wa miaka 16 akamatwa kwa kumuua mtoto wa wiki sita

Mvulana mwenye umri wa miaka 16 ameshtakiwa kwa mauaji kufuatia kifo cha mtoto mwenye wiki sita huko Southampton nchini Uingereza.

Wapelelezi kutoka kituo cha Polisi cha Hampshire walimshtaki kijana huyo siku ya Jumanne usiku baada ya kukamatwa asubuhi ya siku hiyo.

Kijana huyo anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya juu mjini Southampton siku ya leo.

Kukamatwa kwa kijana huyo kulikuja baada ya maafisa na wauguzi wa afya kuwaita Polisi majira ya saa 11 alfajiri ambapo wauguzi waliletewa mtoto huyo kwa ajili ya matibabu na huyo kijana.

Hata hivyo mtoto huyo aliyelepekwa katika Hospitali hiyo kuu huko Southampton alifariki baadaye.

Pia mwanamke mwenye umri wa miaka 18 alikamatwa kwa mashka ya mauaji na bado na Polisi wanaendelea kumchuguza ila sasa ameachiwa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW