Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Mwaka 2018 wageuka neema kwa Lady Jaydee

Mwaka 2018 umeanza kuonekana wa neema kwa Malkia wa muziki wa Bongo Flava, Lady Jaydee.

Baada ya miaka iliyopita kuonekana kukaa kimya kwa kipindi kirefu bila ya kufanya show huku mashabiki wakizidi kumtamani kumuona jukwani, msanii huyo ameonyesha hali hiyo ni tofauti kwa mwaka huu tangu alipopata uongozi mpya wa Taurus Musik.

Jide anatarajiwa kufanya show yake ya pili kwa mwaka huu itakayofanyika Machi 31 katika ukumbi wa Goden Tulip, Oysterbay.

Hilo linatokea ikiwa ni mwezi mmoja umepita tangu alipofanya show yake ya Valentine’s Day iliyofanyika February 10 ya mwaka huu katika ukumbi wa Serena Hotel na kumualika msanii Alicios.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW