Burudani

Mwana FA: Sikuwa najua mapenzi ni nini mpaka Maleeka alipozaliwa

Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amesema alikuwa hajui mapenzi ni kitu gani mpaka pale binti yake aliyetimizia miaka miwili hivi karibuni, Maleeka kuzaliwa.

page

Akiongea na Bongo5, Mwana FA amesema tangu awe na mtoto, maisha yake yamebadilika kwa kiasi kikubwa na kumfanya aishi maisha ya kujilinda zaidi kuliko zamani.

“Nimekuwa very careful, I am worried, siko reckless kama nilivyokuwa. Naogopa nina mtu ananitazama na sitaki kumwangusha. Watu wengine tumekua kidogo juu juu sana, sitaki maisha yangu ambayo mimi nimekua impitie mwanangu hata kidogo,” alisema FA.

“Amenibadilisha, nawaza, nina wasiwasi kuhusu maisha yangu ya mbele. Kiukweli maisha yangu ya kufikiri kuhusiana na maisha na vitu vingine vinavyonizunguka vimebadilika sana kwaajili ya binti.”

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/118085637″ width=”100%” height=”166″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents