Michezo

Mwanachama wa Yanga SC, Ally Yanga azikwa leo (Picha)

Aliyekuwa shabiki maarufu wa klabu ya Yanga SC, Ally Said amezikwa leo nyumbani kwao Mkoani Shinyanga. Shabiki huyo maarufu kwa jina la Ally Yanga alifariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea Mpwapwa, Dodoma Juni 20 mwaka huu.

Jeneza likiwa limebeba mwili wa aliyekuwa shabiki na mwanachama wa Yanga, Ally Yanga

Umaarufu wa shabiki huyo unatokana na mapenzi aliyokuwa akiyaonyesha juu ya klabu yake pamoja na kujipaka masizi na kuweka kitambi alipokuwa akienda kuishabikia timu hiyo katika mashindano mbali mbali.

Jeneza likiwa limebeba mwili wa aliyekuwa shabiki na mwanachama wa Yanga, Ally Yanga

BY  HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents