Habari

Mwanaume wa Iran ambaye hajaoga kwa miaka 60 avunja rekodi, ‘World’s Smelliest & Dirtiest Man Alive’

Mr Amou Haji ni raia wa Iran mweye miaka 80, ambaye amevunja rekodi ya kutooga kwa miaka 60 na kuwa ndiye mwanaume mchafu kuliko wote duniani.

haji-1

Kwa mujibu wa DAILY MAIL, Haji alifanya maamuzi ya kuishi maisha ya uchafu kutokana na kuamini kwamba kuwa msafi kutamfanya aumwe.

Kwa wale single ladies, Haji yuko single na anahitaji mpenzi, lakini mwanamke ambaye atapenda kuwa naye ni lazima akubaliane na lifestyle yake.

haji-3

haji-4

Mr Haji hupendelea kusmoke, na ili arelax hupenda kuvuta kiko chenye kinyesi cha wanyama. Upande wa chakula hupendelea kula nyama zilizooza za wanyama waliokufa, pamoja na maji lita tano kwa siku kwa kutumia kidumu cha mafuta chenye kutu. Chakula anachokipenda zaidi ni Nungu nungu aliyeoza.

Mr. Haji pia anapohitaji kupunguza nywele zake huzichoma kwa moto.

haji-2

Baadhi ya wakazi wa kijiji anachoishi cha Dejgah huko Iran, waliwahi kutaka kumsaidia Haji aweze kuoga, lakini aliwatoroka. Usiku Mr Haqji hulala katika mashimo yanayofana na kaburi.

Rekodi ya mwanaume aliyekaa muda mrefu bila kuoga iliyovunjwa na Mr Haji iliwekwa na mwanaume wa India Kailash Singh (66), aliyeishi bila kuoga kwa miaka 38.


SOURCE: DAILY MAIL

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents