Michezo

Mwenyekiti wa timu ya Schalke 04 ajiuzulu kisa Afrika , mashabiki walani vikali ”Naomba msamaha kwa niaba ya klabu”

Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Schalke 04 ya nchini Ujerumani, Clemens Tönnies amelazimika kujiuzulu nafasi hiyo kwa muda kufuatia matamshi yake ya wiki iliyopita yaliyo ilenga bara la Afrika ambayo yamekosolewa kuwa ya kibaguzi.

Tönnies entschuldigt sich für Äußerung über Afrikaner (picture-alliance/dpa/I. Fassbender)

Licha ya kujiuzulu kwake haionekani kana kwamba matamshi hayo yatamuangusha moja kwa moja.

Akizungumza kwenye mkutano mjini Paderborn alipokuwa akikutana na wageni 1,600 wiki iliyopita, Tönnies mwenye umri wa miaka 63, anaripotiwa kukosoa kuongezwa kwa kodi kwa ajili ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi na kupendekeza kuwa ni heri kujenga viwanda 20 vya kuzalisha umeme kila mwaka barani Afrika.

Tönnies alinukuliwa na gazeti la Neue Westfaliche akisema “Kisha viwanda hivyo vitakapojengwa basi Waafrika wataacha kukata miti na wataacha pia kutafuta watoto wakati wa giza linapoingia.”

Bodi ya klabu imetoa taarifa ya kujiuzulu kwake

Hata hivyo ameomba radhi kwa matamshi yake aliyotoa kwa niaba ya klabu hiyo akiamini kuwa ni ya kibaguzi “ “Samahani kwa maoni yangu juu ya idadi kubwa ya watoto barani Afrika. Kama mwenyekiti wa bodi ya usimamizi wa FC Schalke 04, mimi nina 1,000% nyuma ya maadili ya kilabu yetu. Hii ni pamoja na mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi kwa msingi wa hilo naomba radhi, haikuwa sahihi nilikosea samahani sana.”

Fussball Schalke l Kritik an Aufsichtsratschef Clemens Tönnies wächst (picture-alliance/dpa/T. Rehbein)Clemens Tönnies ni bilionea nchini Ujerumani.

Na sasa baada ya matamshi yake kulaaniwa sana na mashabiki wa klabu ya Schalke, bodi ya klabu hiyo imetoa taarifa na kusema kwamba mwenyekiti huyo amejiuzulu kutoka kwenye wadhfa wake japo kwa miezi mitatu tu kwa kuwa imempata hatia ya kwenda kinyume na sera zinazopinga ubaguzi za klabu hiyo. Bodi hiyo lakini imesema kwamba haioni matamshi yake hayo kuwa ya kibaguzi kwa namna yoyote ile.

Baada ya tangazo hilo mashabiki wa Schalke kupitia kwa mwakilishi wao Susanne Franke wamesema kwamba bila shaka watapinga iwapo mambo yatasalia jinsi yalivyo na uamuzi huo hautobadilishwa na hatua kali zaidi kuchukuliwa dhidi yake.

Wawakilishi wa michezo na hata wanasiasa wamemtaja Tönnies kuwa mtu ambaye hajastaarabika na matamshi yake kama yaliyopitwa na wakati.

Gerald Asamoah ameelezea kuumizwa kwake na matamshi hayo

Mchezaji wa zamani wa Schalke ambaye ni raia wa Ghana Gerald Asamoah, ambaye pia ni kocha wa timu ya Schalke ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka ishirini na tatu, ameelezea kusikitishwa kwake na matamshi hayo akiandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram “nimeshtushwa, nimeghadhabishwa na nimeumia sana, amenitukana mimi na wageni wengine wote, hatuwezi kulivumilia hilo,” mwisho wa kunukuu.

Training FC Schalke 04 (picture-alliance/dpa/Revierfoto)

Gerald Asamoah (kulia) akiwa na Tönnies

Shirikisho la Soka la Ujerumani, DFB, limesema kuwa ni jambo la kushtusha na kusikitisha kuona kwamba mtu mwenye nafasi na uzoefu mkubwa kama Tönnies anatoa matamshi mabaya kama hayo kuhusu watu wa bara zima.

Lakini kocha wa Schalke, Huub Stevens, amemtetea mwenyekiti wake kwa kusema “yeyote anayemjua Tönnies, yeyote ambaye ameshafanya kazi naye kwa muda mrefu, anamfahamu kwamba anapenda watu pasipo kujali rangi ya ngozi, asili wala dini yake.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents