Mwijaku amchana Baba levo baada ya kuikosoa show ya Alikiba, anatumiwa vibaya aliomba ku-perform akakataliwa (+Video)

Msanii wa Bongo movie na Mtangazaji wa Clouds media @mwijaku amemtolea uvivu @officialbabalevo baada ya kumshauri @officialalikiba asogeze show yake mbele akidai ataenda kuumbuka kisa show inafanyika katikati ya mwezi tofauti na ingefanyika mwisho wa mwezi ili apate watu wengi huku kukiwa ni mwisho wa mwezi.

Baada ya kauli hiyo ya @officialbabalevo @mwijaku amesema kuwa @officialbabalevo aliomba akaparform kwenye show hiyo na @officialalikiba amekataa kwa sababu anataka wasanii wa kuimba Live na Baba levo hajazoea show za Live.

@mwijaku akiongea hayo kwenye tukio la @richmavoko akizindua Minitape yake, amemshauri @officialbabalevo kuwa akomae na siasa kwani mambo ya muziki hayawezi.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW