BurudaniHabari

Mzimu wa Nature waitafuna Tmk!

MzimuHuku siku zikiwa zinazidi kusonga…dalili zimeonekana kuwa mbaya zaidi kwa kundi la Wanaume TMK,ambapo mmwishoni mwa wiki msanii mwingine anayekwenda kwa jina la ‘Mzimu’ amejiondoa

MzimuHuku siku zikiwa zinazidi kusonga…dalili zimeonekana kuwa mbaya zaidi kwa kundi la Wanaume TMK,ambapo mmwishoni mwa wiki msanii mwingine anayekwenda kwa jina la ‘Mzimu’ amejiondoa na kukimbilia kundi la ‘Wanaume Halisi’ linaloongozwa na Sir Juma Nature.

 

Kujiondoa kwa msanii huyu ambaye pia ameshiriki kwenye track ‘Kazi tu’,ambayo imekuwa ikitafsiriwa na wengi kama dongo kwa kina Nature…kumekuja miezi michache baada ya kuvunjika kwa kundi hilo kwa maelezo kuwa wanataka haki, ukweli na uwazi kwa ajili ya maendeleo ya wote.

 

Akiongea kama kiongozi wa ‘Wanaume Halisi’,Nature alisema kuwa kwenye ukweli haki haipotei na kwamba anaamini wasanii waliobaki ‘Wanaume TMK’ wanajua ukweli uliopo na ndio maana ‘Mzimu’ ameamua kufwata upepo anaohisi utamletea maendeleo ya kweli na si majungu…huku akisisitiza kuwa hawapendi kuzungumza ya watu lakini mifano itaonekana baadaye,”.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents