BurudaniHabari

Miss Tanzania atakiwa kujieleza

Miss TanzaniaKAMATI ya Miss Tanzania imempa muda Vodacom Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ili kujieleza kwa maandishi kuhusu habari zilizoandikwa katika vyombo vya habari hivi karibuni

Miss TanzaniaNa Suleiman Mbuguni

KAMATI ya Miss Tanzania imempa muda Vodacom Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ili kujieleza kwa maandishi kuhusu habari zilizoandikwa katika vyombo vya habari hivi karibuni.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambayo ndio inayoandaa mashindano ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga, alisema Dar es Salaam jana kuwa kamati yake ilikutana, ambapo ilimwita Wema ili ajieleze.

Alisema baada ya kukutana na Wema aliweza kujieleza, lakini hata hivyo kamati ilimpa muda wa kujieleza kimaandishi na kutakiwa kupeleka maelezo yake katika ofisi za kamati hiyo.

Lundenga alisema kamati yake inafanya mambo kiutawala zaidi, ndio maana imemtaka mnyange huyo kujieleza kimaandishi kwa kuwa hawafanyi kazi kwa kutumia vyombo vya habari.

“Hatuwezi kumhukumu bila ya yeye mwenyewe kujieleza, pengine aliyepeleka habari hizo nje ni mtu ambaye alikuwa nae na kwa nini asiulizwe rafiki yake wa kiume, labda ndio yeye aliyezitoa habari hizo?” alihoji Mkurugenzi huyo.

Alisema Wema ni mtu mzima, ambaye amefikisha miaka 18, anapaswa na kuwa rafiki wa kiume kama binadamu kawaida na picha zilizochapishwa kwenye vyombo vya habari zinaonekana zilipigwa ndani, ndio maana kamati yake imempa muda wa kujieleza.

Hata hivyo Lundenga ambaye hakusema Kamati yake imetoa muda gani, alisema si kwamba anamtetea mnyange huyo, bali anataka mambo hayo kuyachukulia kiutawala kama ambavyo katiba yao inavyowaelekeza.

Wiki iliyopita baadhi ya magazeti yalichapisha picha za Wema akiwa na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed ‘TID’, wakiwa pamoja chumbani katika hali ya kimapenzi.

Pia mrembo huyo mwaka jana aliiweka familia yake katika hali ya wasiwasi baada ya kutoonekana nyumbani kwao kwa siku nzima, hatua ambayo iliwalazimu wazazi wake kutoa taarifa polisi.

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents