Burudani

Nahitaji wasanii wa kike – Barnaba

Msanii wa muziki Bongo, Barnaba amesema mwakani anahitaji kuanza kuchukua wasanii kwa ajili ya label yake ila wa kike pekee.

Muimbaji huyo ameiambia 5 Selekt, EATV kuwa anahitaji wasanii wa kike watatu kwani wa kiume tayari wapo wengi katika game.

“Mimi label yangu ni changa hata mwaka jana nilisema nitatambulisha wasanii, mwakani nitamtoa (Mula) na nitaanza kuchukua chapa nyingine na in fact nimesema nahitaji wasanii wa kike sana, nahitaji wa kike watatu tu” amesema Barnaba.

“Kwa hiyo wa kiume atabaki Mula pekee na ni sababu ya msingi sana wanaume tupo wengi sana, halafu nimeamua kufanya hivyo kwa sababu mimi ni mwandishi mara nyingi nyimbo zangu zinawiana kwa mabinti na nimeamua kuja hivyo, am sure mtu kama Diamond ameshasaidia sana” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents