Burudani

Nay ashambuliwa na mzazi mwenzake kuhusu matunzo ya mtoto

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Nay wa Mitego amechezea kichambo kutoka kwa anayedaiwa kuwa mzazi mwenzake ambaye ni muigizaji wa filamu, Skyner Ally kwa madai ameshindwa kuwa baba bora kwa binti yake.

Skyner Ally akiwa na mtoto wake aitwaye, Munie

Hatua hiyo imekuja baada ya rapa huyo hivi karibuni kumpost mtoto wa kike wa binti huyo na kuwataka vijana kukaa naye mbali.

Ujumbe na Nay wa Mitego

Baada ya mama wa binti huyo kuona ujumbe huo, amefunguka mengi kuhusu Nay wa Mitego huku akidai kumshangaa kwa nini amefanya kitendo hicho wakati hataki kutoa huduma kwaajili ya mtoto.

“Thats face you make when you see your ‘daddy jina’ anakufanyia promotions na kudanganya Watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi unayovaa hajui thamani yake maskini. Nimevumilia sana it’s 5 Years now nimejiskia kutapika na nimetapikaa. Am done Mungu wa mbinguni nakuomba unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki….. uzima wa afya nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake” aliandika Skyner kupitia Instagram.

Aliongeza “Endelea na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki…Please unapost picha za mtoto wangu za nini…shobo dundo zanini? Sitaki shobo na mwanangu koma kama ulivyo komaaa…Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done”

Skyner hakuishia hapo aliendelea kutoa husia kwa binti yake kwa kuonyesha jinsi alivyo na umuhimu katika maisha ya binti yake

“Hakuna anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba’ko hana analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy Birthday My Happiness,” alisema Skyner.

Hata hivyo rapa huyo bado hajazungumza chochote kuhusu sakata hilo, Bongo5 bado inafanya jitihada za mtafuta.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents