Burudani

Ndoa ya Lulu na Majay yanukia

Elizabeth Michael (Lulu) amedai ndoa yake na mpenzi wake Dj Majay inakaribia.

Muigizaji huyo ambaye ameonekana kutulia sana tangu alipokuwa na mahusiano na bosi huyo wa EFM na TVE amesema hivi karibuni wale waliokuwa wakitaka waachane watabaki midomo wazi.

“Siku zinakaribia na karibu tarehe ya ndoa yangu itatangazwa kwa uwezo wa Mungu. Hapo ndipo waliotamani tuachane wataziba midomo, maana natarajiwa kuwa mke halali hivi karibuni,” ameliambia gazeti la Mtanzania.

Lulu ameongeza kuwa anatamani kuwa mke bora kwenye ndoa yake kama alivyokuwa sasa kwenye mahusiano yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents