Burudani ya Michezo Live

Ndoa ya Mbunge wa Segerea, ‘Bonnah Kaluwa’ yavunjika, mwenyewe afunguka ‘mambo ni mengi na muda ni mchache’

Mbunge wa jimbo la Segerea Jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Mhe. Bonnah Kaluwa amethibitisha kuwa kwa sasa hayupo kwenye mahusiano baada ya kuachana na aliyekuwa mumewe, Moses Kaluwa.

Bonnah Kamoli

Taarifa za kuachana kwao zilianza kusambaa mitandaoni ambapo, Mhe. Bonnah alianza kubadilisha jina lake kwenye kurasa zake zote za mitandao ya kijamii, ambapo alibadilisha jina llililozoeleka la Bonnah Kaluwa na kuandika jina la Bonnah Ladslaus Kamoli.

Hata hivyo, wakati akihojiwa na Gazeti la Mwananchi, amesema kuwa “Taarifa hizo ni za kweli” na sababu ya kuachana ni matatizo ya kifamilia.

Ni matatizo ya kifamilia..nimeshaweka majina yangu kwenye mitandao ya kijamii. Nimeweka Instagram, Facebook. Bunge wana taratibu zao, si wamepata barua? Mimi nimepata yangu nimebadilisha,” amesema Mhe. Bonnah .

Gazeti hilo, limedai kuwa Kampuni ya uwakili ya Carmel Attorney inayomsimamia aliyekuwa mume wa Donnah, imethibitisha kumwandikia barua Bonnah na nyingine kupeleka Bungeni kumzuia kutumia jina la Kaluwa.

Tayari Mbunge huyo, ameanza kutema cheche kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya taarifa hizo kuvuja kwa kuandika “Jamani kwani kuna habari huko.jamaniii.basi ndio hivyo mambo ni mengi na muda ni mchache“.

Chanzo: https://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/Mbunge-Bonnah–Kaluwa–akiri-ndoa-yake-kuvunjika/1597296-5000242-l1ppys/index.html

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW