Michezo

Ndoa ya Tiger Woods ‘No More’

Mchezaji namba moja wa golf duniani Tiger Woods na mkewe Elin Nordegren wametangaza rasmi kuvunjika kwa ndoa yao na wawili hao kuachana.

 

“Tunasikitika kuchukuanafasi hii kutangaza kuwa ndoa yetu imevunjika rasmi” ilisema taarifa iliyotolewa kwa pamoja na wanandoa hao juzi.

Katika taarifa hiyo Tiger Woods na mkewe walisema watapeana majukumu ya kuwalea watoto wao wawili kwa pamoja. Ingawa taafira zaidi ya kuvunjika kwa ndoa hiyo haikusema lolote kuhuso mgawanyo wa mali habari zinasema kuwa mke wa Tiger ataondoka na kititita cha dola za kimarekani million mia moja.

Ndoa hiyo ilivunjwa mbele ya jaji Jidy Pittman Biebel na mahakaya ya Bay Circuit mjini Florida,kufuatia wanawake mbalimbali kujitokeza na kudai kuwa na mahusiano nje ya ndoa na Woods.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents