Habari

Ndoani kuna nini kwa mastaa? Sio Oprah peke yake, hata P. Diddy hafikirii kuoa

Kumbe sio Oprah peke yake ambaye swala la kuingia kwenye ndoa haliko katika mipango yake, star mwingine wa hip hop na mwanzilishi wa Bad Boy Records Sean John Combs aka P.Diddy naye wala hafikirii kuoa.

Diddy-and-Cassie-GQ-Party
Diddy na girlfriend wake Cassie

Diddy (43) ni mmoja kati ya wasanii wa hip hop ambao ni wazazi, na anaonekana kuwa baba bora kwa wanae Christian Casey Combs, Justin Dior Combs, Chance Combs, na mapacha D’Lila Star Combs na Jessie James Combs. Kupitia Instagram Diddy amekuwa akipost picha nyingi za binti zake watatu anaoonekana kuwapenda zaidi na kuelezea kiasi anachowapenda.

Diddy na binti zake
Alipost picha hii Instagram na kuandika ‘My 3 little super models #ProudDad …I’m really in trouble! No for real. No dating till you’re 25!!! Haa lol’

Upande wa Oprah alikuwa na sababu zake za kwanini hana mpango wa kuolewa japo amekaa miaka mingi sana na boyfriend wake Stedman Graham, alisema ndoa ina majukumu ambayo anadhani kama mke asingeweza kuyatimiza.

Upande wa Diddy ambaye pia ameanzisha TV Channel yake Revolt Television Network, akiongea kwenye talk show ya The View ya ABC TV amesema,
“Nadhani watu wengi wanaweka nguvu nyingi sana ya kuingia kwenye ndoa badala ya kuweka nguvu nyingi katika kutafuta furaha….Mimi nina furaha, na kila mtu ambaye yuko katika maisha yangu ana furaha. Ninahitaji tu kuwa na furaha na nadhani ni muhimu kwako kuilinda furaha yako na kujipenda mwenyewe, kwasababu baada ya hapo unaweza kuwapenda na watu wengine”.

Aliongeza kuwa hatazamii kuingia kwenye ndoa kwasababu anajua majukumu ambayo huja na ndoa, na anadhani kuwa watu wengi hurukia ndoa lakini sio waaminifu.

“Mimi najiamini, sitaki kuoa halafu nishindwe kumfanya mwanamke niliemchagua ajione ndiye bora. Nakaribia huko, na nitakapokuwa tayari nitatangaza, na ntakapoamua kufanya basi ndio itakuwa moja kwa moja”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents